Hosea 4:6-19

6 awatu wangu wanaangamizwa
kwa kukosa maarifa,

“Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,
mimi nami nitakukataa wewe
usiwe kuhani kwangu mimi;
kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako
mimi nami sitawajali watoto wako.
7 bKadiri makuhani walivyoongezeka,
ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu,
walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu.
8 cHujilisha dhambi za watu wangu
na kupendezwa na uovu wao.
9 dHata itakuwa: Kama walivyo watu,
ndivyo walivyo makuhani.
Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zao
na kuwalipa kwa matendo yao.

10 e“Watakula lakini hawatashiba;
watajiingiza katika ukahaba
lakini hawataongezeka,
kwa sababu wamemwacha Bwana
na kujiingiza wenyewe
11 fkatika ukahaba,
divai ya zamani na divai mpya,
ambavyo huondoa ufahamu
12 gwa watu wangu.
Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti
nao hujibiwa na fimbo ya mti.
Roho ya ukahaba imewapotosha,
hawana uaminifu kwa Mungu wao.
13 hWanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima
na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima,
chini ya mialoni, milibua na miela,
ambako kuna vivuli vizuri.
Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba
na wake za wana wenu uzinzi.

14 i“Sitawaadhibu binti zenu wakati
wanapogeukia ukahaba,
wala wake za wana wenu
wanapofanya uzinzi,
kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya
na kutambikia pamoja na makahaba
wa mahali pa kuabudia miungu:
watu wasiokuwa na ufahamu
wataangamia!

15 j“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli,
Yuda naye asije akawa na hatia.

“Usiende Gilgali,
usipande kwenda Beth-Aveni
Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

Wala usiape,
‘Hakika kama Bwana aishivyo!’
16 lWaisraeli ni wakaidi,
kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi.
Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga
kama wana-kondoo
katika shamba la majani?
17 mEfraimu amejiunga na sanamu,
ondokana naye!
18 nHata wakati wamemaliza vileo vyao
wanaendelea na ukahaba wao,
watawala wao hupenda sana
njia za aibu.
19 oKisulisuli kitawafagilia mbali
na dhabihu zao zitawaletea aibu.
Copyright information for SwhNEN